31 Julai 2014 - 09:13
kiongozi wa mapinduzi ya Iran: niwadhifa wa  walimwengu wote hasa waislamu kuwapatia  silaha wapalestina

kiongozi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran Sayyed Ally Khaminiy amesema: suala la palestina ni suala la kwanza muhimu katika ulimwengu wa kiislamu na walimwengu wote wanapaswa kutafuta njea ya kuwapatia silaha wapalestina, kinyume na wanavyodai baadhi ya viongozi wa kimarekani kuwa kikundi cha Hamasi na Jihadi vinapaswa kunyang`anywe silaha

Shirika la habari AhluBayt (a.s) ABNA: kiuongozi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo alipokuwa akihutubu hutuba ya pili ya sala ya Eidil Fitri katika mji mkuu wa Tehran akisema: suala la Palestina ni suala la kwanza muhimu katika ulimwengu wa Kiislam pia ni suala la kwanza kwa wapenda haki ulimwengu mzima, aidha alisema mbwa mwetu wala watu wamevamia wanadamu dhaifu wasio na nguvu nakusema  ivi nani mwenye kudhulumiwa zaidi kuliko vitoto vichanga vyakipalestina vinavyo uwawa na mabomu ya utawala wa kidhalimu wa kizayuni? Nani anayedhulumiwa zaidi kama akina mama ambao huona watoto zao wakisukuma miguu na kukata roho mikononi mwao haliyakuwa hawana jinsi yakufanya katika kuwaokoa watoto zao, utawala wa kizayuni wafanya jinai hizo mbele ya macho ya walimwengu wakikiuka ubinadamu na haki za binadamu, hivyo watu wapenda haki waliokuwa na ubinadamu wanapaswa kutoa majibu nakupambana na vitendo hivyo vichafu dhidi ya ubinadamu.
Alisema kuna nukta tatu muhimu katika suala zima la Gaza nilazima kulifahamu: nukta ya kwanza nikwamba wanachofanya wazayuni katika ukanda wa Gaza ni mauaji ya kimbali ambayo yanalenga kuangamiza taifa la Palestina na nitukio la kihistoria  ampo watendaje wa mauaji hayo na wale wanaosaidia nakuunga mkono mauaji hayo nilazima wahukumiwe kimataifa, hukumu ya mafasidi hao inapswa isimamiwe na wapenda haki na wanasulhu wa kimataifa, alisema tunapozungumzia hukumu ya watu hao haihusu zama maalumu kwamaana wanapaswa kuhukumiwa sawasawa katika zama za utawala wao au baada ya utawala wao na alimalizia kusema kuwa hukumu hiyo inakusanya hata walie wanaowaunga mkono kwa wazi waovu hao.
Ama nukta ya pili: nakwamba watu wanapaswa kuzingatia uwezo wa mwanadamu katika stahamila na uvumilivu wa mambo, kwani wananchi na jeshi linalosimamia haki katika ukanda wa Gaza pamoja yakuwa hakuna uwiano kijeshi baina yao na wazayuni lakini bado wanapambana kutetea haki zao, wananchi ambao wamezungukwa kila pande na jeshi la adui mzayuni wakishambuliwa katika kila pande upande wa bahari, nchi kavu na anga pia mipaka yote imefungwa, katika ambayo hawana maji safi, kukatiwa umeme nk , haya yote ni mafunzo kwetu kwamba mwanadamu anauwezo mkubwa sana katika kutetea haki yake, hasa pale mama anapoona mwanae akifariki mbele yake, pia baba humuona mtoto akitokwa na roho, haya humfanya mwanadamu kupata nguvu zaidi katika kutetea haki, nami bilahska nawabashiria kuwa ushindi utakuwa kwa Wapalestina nakupata hakizao za msingi, kama munavyoshudia kuwa sasa wamekwama na hawajui wafanye nini ndiomaana waona washirika wao wanajitahidi kuwalazimisha Wapalestina kusimamisha vita kwalengo la kumuokoa mzayuni katika hali alionayo kwani hatima ya ushindi ni kwa Wapalestina.
Nukta yatatu, nikwamba sisi bilashaka tuko tofauti na viongozi wa kisiasa za kibeberu ambapo wanasema kuwa Hamasi na Jiadi wanyang’anywe silaha ambapo wakikusudia kwamba hivi sasa kwa uchache Wapalestina wanamiliki idadi chache ya silaha ambazo kwa kiasi fulani wanaweza kujitetea, ama wao hawapendi kuona hali hiyo bali wanatamani kuwa Wapalestina wasiwe na kitu chochote cha kujitetea kiasi kwamba wazayuni muda wowote wakiamua kufanya kitu chochote waweze kufanikisha pasina kikwazo chochote, kwani Rais wa Marekani ametua tamko kwamba wanajeshi wanaojitetea wa Palestina wanyang`anywe silaha, ama sisi tunasema nakusisitiza kinyume chake kuwa walimwengu wote hasa Waislamu niwadhifa wao wajitahidi kwa jinsi wawezavyo katika kuwasaidia Wapalestina kumiliki silaha nzito zaidi na yenye kiwango cha hali ya juu.
Mwisho alimuomba Mungu nakusema: Ewe mwenyezi Mungu Mola wetu unusuru Uislamu na Waislamu, yanusuru majeshi ya Kiislamu, wadhalilishe makafiri na wanafiki na wapinga haki.